Afisa mtendaji mkuu wa bodi ya Ligi Boniface Wambura ametangaza ratiba rasmi ya Ligi Kuu soka Tanzania Bara ambapo Ligi Kuu itaanza Septemba 12 2015 ambapo itakuwa ni wiki moja baada ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kucheza na timu ya taifa ya Nigeria mchezo wa kufuzu AFCON 2017.

Ratiba ya Kombe la FA
itatoka baada ya kutoka kwa ratiba za Ligi daraja la kwanza na Ligi
daraja la pili kwani timu shiriki zinategemea viwanja ambavyo pia
vitatumika katika michezo ya Ligi Kuu.
“Msimu wa
Ligi umeshafunguliwa kwa maana ya usajili ila kwa mashindano na tutaanza
kucheza Septemba 12 na tutamaliza mzunguko wa kwanza Novemba 7 baada ya
hapo tutaingia katika usajili wa dirisha dogo kupisha michuano ya Challenge Cup na tutaendelea December 19 na tutaenda kumaliza Ligi Mei 7 2016″
Hii ndio ratiba yote ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2015/16.

0 comments