Thamani ya Yuan ya China imeshuka kwa asilimia 3.5 dhidi ya Dollar kwa siku mbili mfululizo ambacho ni kiwango kikubwa zaidi kuwahi kutokea kwa miongo kadhaa sasa

Jumanne Benki ya Watu wa China ilishangaza ulimwengu kwa kutekeleza uangushaji wa sarafu yao kwa asilimia mbili

hatua hiyo imeshtua masoko makubwa huku wamarekani wakihofia itaathiri uchumi wao
Inasemekana China imekusudia kuishusha sarafu yao ili iweze kushusha gharama zake za usafirishaji bidhaa kwa mataifa mengine

China imedai kuwa imebadilisha sera yao yakifedha iliwaweza kuwa na nguvu kimasoko kwa miaka ijayo na waweze kuidhbiti hela yao vizuri.