Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez (kushoto), akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam jana kwenye
mkutano juu ya kampuni ya Tigo kuanza kutumia mfumo wa kwanza Afrika wa
mawasiliano ya 4G DVNO ikishirikiana na Uhuru One.
|
Mkurugenzi Mkuu wa mradi huo Uhuru One,
Rajab Katunda (kushoto), akizungumza katika mkutano huo kuhusu mradi
huo. (katikati) ni Meneja Mradi huo wa Tigo, Kobbina Awuch.
Meza kuu. Kutoka kulia ni Ofisa Mtendaji
Mkuu wa Uhuru One, Baraka Mtunga, Mkurugenzi Mkuu wa Mradi huo kutoka
Uhuru One, Rajab Katunda, Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez na Meneja Mradi huo wa Tigo, Kobbina Awuch
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano ukiendelea.
KAMPUNI ya Tigo imeanzisha mfumo wa
kuunganisha mtandao wa 4G LTE kwa wateja wa mtandao huo na wakazi wa Dar
es Salaam kwa lengo la kuboresha mawasiliano.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar
es Salaam jana, Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Diego Gutierrez alisema
upanuzi wa 4G umetokana na mafanikio yaliyopatikana katika awamu ya
majaribio yaliyofanywa na kampuni hiyo maeneo ya Mliman Cioty na Masaki
Peninsula Aprilmwaka huu.
Alisema upatikanaji wa 4G jijini kote
unaridhisha na kwamba dhamira ya tigo ni kuendeleza mageuzi ya
kidijitali nchini na kuongoza katika utoaji wa huduma zaidi na za
uhakika kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa wateja.
Gutierrez alisema mtandao wa 4G LTE
unamaanisha ongezeko la kasi ya kuperuzi na kupakua habari kutoka kwenye
intaneti, kupiga simu kwa njia ya skype. pia inamwezesha mteja kupata
mtiririko wa video au kufanya mkutano kwa njia ya mtandao kwa ubora wa
hali ya juu.
"Upanuzi huu unamaanisha wateja wa tigo
waliopo katika wilaya za Kinondoni, Ilala na Temeke waishio maeneo ya
Upanga, Posta, Tegeta, Mbagala, Tabata, Kimara, Mbezi, Ukonga, Salasala,
Mikocheni, Msasani, Sinza sasa watapata huduma bora na upatikanaji wa
intaneti ya kasi zaidi kupitia mtandao wetu,"alisema Gutierrez.
Aliongeza kuwa kampuni hiyo ipo mbioni
kuzindua huduma ya 4G katika miji ya Arusha , Dodoma, Morogoro, Moshi,
Mwanza na Tanga mwezi ujao na hivyo kuifanya kampuni hiyo kuwa na
mtandao mkubwa na wa kasi zaidi wa 4G nchini.
Wakati huohuo kampuni hiyo imeanzisha
ushirikiano na kuunda mfuno wa utoaji huduma za kimtandao usiotumia
muindombinu asilia ya mawasiliano ambao utaiwezesha UhuruOne kupanua
upatikanaji wa teknolojia ya 4G na kwamba mfumo huo ni wa kwanza barani
Afrika.
0 comments