Bendi ya Yamoto bendi Chini ya Mkubwa na wanawe na ile ya Malaika bendi chini ya Christian Bella zatumbuiza Usiku wa Masauti Luxury katika ukumbi wa Millenium Tower na kuwaacha waliohudhuria wakiwa na kiu ya burudani zaidi.

Bendi ya Yamoto bendi ilikuwa ya kwanza jukwaani wakitamba na vibao vyao marufu kama vile Naenda kusema kwa Mama na kile chenye mistari ya .....unarambooo....... .....nina muwa... na vingine huku wakimiliki jukwaa kwa zaidi ya masaa mawili kuhakikisha wanawaridhisha mashabiki wao waliohudhuria kwenye sherehe hio.

Christian Bella na Bendi yake ya Malaika bendi walikuwa wa mwisho kumiliki jukwaa wakiwatumbuiza halaiki ya watu kwa vibao vyao vikali kama vile Nani kama mama, Msaliti na vingine vilivyowanyanyua mashabiki wao waliohudhuria kwenye usiku huo. 

  
 wasanii wa Yamoto Bendi wakitumbuiza halaiki ya watu katika usiku wa Masauti Luxury  leo.

 Christian Bella na Bendi yake wakitumbuiza katika usiku wa Masauti LUxury leo.

T.I.D. Mnyama na Qchief wakipata burudani kutoka kwa bendi ya Malaika inayoongozwa na Christian Bella