Wananchi na kiu ya 'Mabadiliko'
Logo of the Kenya African National Union
Nembo ya Chama Cha KANU
 1. November 2, 1991 wananchi wa Zambia walimchagua Ndg. Chiluba ambaye alimshinda aliyekuwa rais kwa zaidi ya miaka 27 na mpigania uhuru wa nchi hiyo Mzee Kaunda; pamoja na sababu zingine ila kubwa zaidi, wananchi hao walihitaji "Mabadiliko".


2. Dec. 2002 chama kikongwe Africa cha KANU chini ya Rais MOI (M o One) kilishindwa vibaya sana na muungano wa NARC chini ya Mwai Kibaki kwa sababu wananchi walihitaji "Mabadiliko"...

Africa hakuna chama kilichokuwa na nguvu kubwa kama KANU. KANU ilisifika kwa kujenga nchi mpaka wimbo maalum wa kitaifa ulitungwa kwa ajili ya kuisifu KANU... "KANU yajenga Nchi".... Ila wananchi walihitaji mabadiliko wakaziba masikio na kufumba mambo...

3. Sep. 2011 Michel Sata pamoja na uzee wake alimshinda Rupia Banda kwa sababu wananchi walihitaji "mabadiliko".....

Ukisoma kitabu cha Dambisa Moyo "Why Zambia" anakueleza vizuri sana jinsi Banda kipindi akiwa rais alijitahidi sana kujenga miundombinu (hasa barabara) mpaka vijijini.

Ila kwa bahati mbaya wananchi hawakuona haya yote kwa sababu ndani ya mioyo yao walisukumwa na hitaji kuu ambalo ni "Mabadiliko"


4. 2012, Macky Sall alishinda uchaguzi wa Senegal na kumbwaga mkongwe wa siasa za Africa Abdoulaye Wade mtu aliyekaa madarakani zaidi ya miaka 20. Kwa hakika haikuwa jambo jepesi wala kazi nyepesi lakini kwa kuwa wananchi walihitaji "mabadiliko" Rais Sall alishinda kwa zaidi ya asilimia 65%....


5. 2015 pamoja na kutukanwa juu ya umri wake, afya yake, na familia yake Ndg. Buhari aliibuka mshindi na kumgaragaza rais aliyekuwepo madarakani (sitting president) G. Jonathan kwa sababu wananchi walihitaji "mabadiliko"..

Nakumbuka Gavana wa Itiki Ndg. Fayose alizunguka nchi nzima ya Nigeria akimtukana Buhari na kusema haifiki siku ya uchaguzi Buhari atakuwa amekufa. Ila leo hii tunashuhudia rais mpya wa Nigeria ni Buhari....


6. Pagan Amum (SG) wa SPLM, South Sudan aliwahi kusema kwamba, inafikia kipindi mabadiliko katika nchi yoyote ile hayakwepeki. Wananchi wanapodai mabadiliko haijalishi umewafanyia mazuri kiasi gani au mabaya kiasi gani ila kikubwa kwao ni kupata mabadiliko.....

Wananchi wanapotaka mabadiliko haijalishi na hawaitaji kujua yatakuwa mabadiliko ya namna gani, ila kikubwa kwao ni kupata mabadiliko...

Wananchi wanapohitaji mabadiliko hawahitaji kujua kama yatakuwa positive kwao au negative kwao wenyewe wanachokijua kwa wakati huo ni kupata mabadiliko....

Wananchi wanapohitaji mabadiliko alyways wanaziba masikio na kufumba macho... Ukiwa chama dola hata uwambie nitakuletea maziwa mlangoni kwako kamwe hawezi kukusikia.... Na akiwa kijana hata ukimuahidi kumpatia msichana mzuri sana kama Cinderela au Cleopatra hawezi kukuelewa... Kikubwa kwake ni kupata mabadiliko... 


Chanzo hakijulikani, iwapo wewe ndio mwandishi wa chapisho hili tunaomba utataarifu ulitufanye masahihisho a chan.