Miss World Tanzania 2014 Happiness Watimanywa
Kamati ya Maandalizi ya Michuano ya Miss Tanzania  imekuja na mikakati ya kurejesha hadhi na heshima ya mashindano hayo ya kusaka walimbwende nchini.
 Hili limekuja baada ya kufunguliwa kwa mashindano ya kumtafuta Miss Tanzania na Baraza la Sanaa la Tanzania (BASATA),
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino Agency, Hashim Lundenga leo ametambulisha mbele ya waandishi wa habari kamati mpya yenye wajumbe 12, ambayo itakuwa inaratibu mashindayo hayo kwa sasa.

miss tz
Wanakamati  wakizungumza na waandishi wa habari
Kamati Mpya ya Miss Tanzania inaundwa na ..........
1.Juma Pinto – Mwenyekiti
2.Lucas Rutta – Makamu Mwenyekiti
3.Doris Mollel – Katibu Mkuu
4.Jokate Mwegelo – Msemaji wa Kamati
5.Hoyce Temu – Mjumbe
6.Mohamed Bawazir – Mjumbe
7.Gladyz Shao – Mjumbe
8.Magdalena Munisi 0 Mjumbe
9.Shah Ramadhani – Mjumbe
10.Hamm Hashim – Mjumbe
11Khalfani Saleh – Mjumbe
12.Ojambi Masaburi – Mjumbe
Kwa upande wa Sekretariet tunao wajumbe 4 ambao ni
1.Dr.Ramesh Shah
2.Hidan Ricco
3.Yasson Mashaka
4.Deo Kapteni

 Lundenga amesema kuwa kamati hiyo inayoanza kazi zake hii leo, itashughulikia mapungufu yote yaliyojitokeza na kurejesha imani ya wananchi kwa mashindano hayo ikishirikiana kwa karibu na wadau mbalimbali pamoja na Basata.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutambulishwa msemaji wa Kamati hiyo, Jokate Mwegelo ametoa shukrani kwa niaba ya kamati yake kwa kuamininiwa kupewa jukumu hilo na kuahidi maboresho makubwa na mikakati endelevu ya kurejesha hadhi ya Miss Tanzania.