Memphis curls in another fine finish.

Mshambuliaji hatari raia wa Uholazi aliyesajiliwa na timu ya ManU msimu huu ametakata leo usiku baada ya kuwaadhibu wapinzani wake kwa kuifungia timu yake mabao mawili na kutoa pasi ya goli.
Mephis 21 alionekana kuwa mwiba kwa mabeki wa timu ya Club Brugge nakufanikiwa kuchungulia lango la timu hiyo mara mbili huku akikosa nafasi ya wazi.
Mabao ya ManU yalifungwa dakika ya 13 na 42 kupitia mshambuliaji wake Mephis na kiungo Fellaini akifunga katika dakika ya 90.Bao la kufutia machozi la Club brugge lilikuwa la kujifunga na kiungo wa Man U Michael Carrick katika harakati za kuokoa dakika ya nane ya mchezo mpira uliopigwa na Victor Vazquez.

Hadi mwisho wa mchezo Man Utd 3-1 Club Brugge














 Na, Raphael Ebacha