Serikali Yakanusha Tena Taarifa za Jenerali Mwamunyange Kuwekewa SUMU...... Yalaani Wanaoponda Rais Kikwete Kuteua Wakuu Wapya wa Wilaya


Wakati  kukiwa kuna taarifa zinazoenezwa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii zikisema mkuu wa Majeshi  ya ulinzi  nchini Jeneral Davis Mwamunyange   amewekewa sumu na hali yake sasa hivi ni  mbaya, huku taarifa hizo zikisema sababu ya kuwekewa  sumu imetokana na masuala ya kisiasa,hatimaye Serikali imeibuka kwa  mara  nyingine  na kukanusha taarifa hizo na kusema ni za uongo zenye nia ya kufakaranish
 
Akikanusha Uvumi huo leo Jijini Dar es Salaam  wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Afisa Habari wa Serikali ambaye pia ni mkurugenzi wa Idara ya Habari –Maelezo Assah Mwambene amesema Jenerali Mwamunyange yupo salama na anaendelea na kazi zake,akidai kuwa taarifa hizo zinalengo  la kuchonginisha watanzania na jeshi na kuharibu picha ya Amani na utulivu uliopo nchini.
  
Mwambene amewataka Watanzania kupuuza taarifa hizo huku akiwasihi kutoingiza siasa kwenye masuala nyeti ya nchi ikiwemo jeshi,kwani jeshi ni taasisi isiyojihusisha na siasa.
 
Wakati huo huo pia Serikali imetolewa ufafanuzi juu ya taarifa  zilizoandikwa kwenye Gazeti la Tanzania Daima  ambazo zilikuwa zinaubeza  uteuzi uliofanywa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete kwa kuwateua wakuu wa wilaya wapya, wakidai uteuzi huo ulikuwa ni   wakulipa fadhila kwa wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM.
 
Akifafanua uteuzi huo, Mwambene amesema watu wanaobeza  uteuzi huo watakuwa hawajui sheria za nchi na kufahamu mamlaka ya Rais.
 
Amesema kwa mujibu wa sheria,kanuni za nchi  na taratibu  Rais anamamlaka  ya kufanya uteuzi  wakati wowote inapobidi kwa malengo ya kuboresha utendaji wa kazi  serikalini.
 
“Serikali imesikitishwa na taarifa zilizotolewa na gazeti la Tanzania daima kuhusiana na uteuzi  wa Rais,taarifa hizi ni za kichochezi na zinalenga kumchonganisha Rais na wananchi wake”amesema Mwambene.
 
Aidha,Mwambene amevitaka vyombo vya habari nchini kufanya utafiti na kusoma kabla ya kuandika habari na pia  akaviasa kuandika habari zenye lengo la kujenga umoja na mshikamano badala ya kuandika habari zenye lengo  la kuwagawa Watanzania.

Chanzo: Fullhabari