Mbunge wa jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe na Capt. William Slaa (baba yake Jerry Slaa), wamethibitika kupoteza maisha kwa ajali ya helkopta katika  eneo la Msolwa, hifadhi ya Selous.

Deo anakuwa mbunge wa sita kupoteza maisha katika kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu. Miongoni mwa waliotangulia ni Dk Emmanuel Makaidi, Dk Abdalla Kigoda, na Mchungaji Christopher Mtikila ambao wameacha vinywa vya waTanzania wengi wazi wakiwa na maswali mengi bila majibu.

Jerry Slaa, ameandika ujumbe kwenye Instagram kuhusu msiba huo uliolifika taifa.

"Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa rasmi kutoka kwa timu ya uokoaji imefanikiwa kufika eneo la ajiali na kukuta abiria wote na rubani wamepoteza maisha"

"Nimempoteza Baba na rubani mzuri wa nchi yetu Capt.William Silaa,nimepoteza rafiki na kiongozi wangu Mhe.Deo Filikunjombe. Nawapa pole wote waliopoteza ndugu zao. Nawaombea marehemu mapumziko ya Amani"

"Nawashukuru wote walioshirikiana na familia kusaidia uokozi.
Namshukuru Mhe.Rais Jakaya M Kikwete, Dr.John Pombe Magufuli, IGP Ernest Mangu, Katibu Mkuu MU Dr.Meru, Kampuni ya Everest Aviation ,Wabunge, MaDC, Maafisa wa TCAA na wote walioshiriki kuwatafuta wahanga wa tukio hili"