Wanajeshi wasiopungua 50, watunza amani wa Muungano wa Afrika, wengi wao kutoka Uganda, wanasadikika kuuawa kwenye shambulio, lililofanywa siku ya Jumanne dhidiya wapiganaji wa Al shabaab katika kambi ya Jannale,iliyoko kilomita 115 Kusini mwa mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Wakaazi wa wilaya hiyo wamethibitisha kuwa kambi hiyo ilishambuliwa na wapiganaji hao wa Al Shabaab.
Wanasema wameona helikopta za kijeshi mapema hii leo ikiwatafuta wanajeshi waliopotea katika maeneo ya mashambani na pia kuwauliza wakaazi hao ikiwa wamewaona wanajeshi wa AU wakiwa hai au wakiwa wameuawa.
Ambapo miili ya wanajeshi watatu ilipatikana karibu na kijiji hicho.
Baadhi ya wanajeshi walikutwa hai ilhali wengine wakiwa wamekufa
  
Wanajeshi hao wa AU nchini Somalia wanakabiliwa na wakati mgumu katika operesheni hiyo baada ya daraja linalounganisha mji huo kuharibiwa kwa mabomu hapo jana.
Hali imeanza kutulia mjini humo lakini wakaazi wanaamini kuwa zaidi ya wanajeshi 40 hawajulikani waliko.
Makao makuu ya kikosi cha Muungano wa Afrika nchini Somalia, AMISOM, imethibitisha kuwa waliwapoteza wanajeshi kadhaa kutoka Uganda ila idadi yao haijajulikana.

                                                                                                                                               chanzo; BBC