Papa Francis wa Kanisa Katoliki

Kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki Papa francis ameelezea kuwa anavaa msalaba uliovaliwa na padre wa Iraqi aliechinjwa.

Alisema alipewa na kiongozi mwingine wa kanisa hilo waliekutana katika kanisa la St.Peter's Square.

"Ni msalaba mchungaji huyu alikuwa ameushikilia mkononi wakati koromea lake linakatwa kwa imani yake yakukataa kumpinga Kristo" Papa Francis alisema hayo akiwahutubia watawa wachanga wa kanisa katoliki.
Aliongezea pia "Huu msalaba nauvalia hapa" akiashiria shingo lake.

Papa Francis ambae  mara kwa mara amezungumzia kuteswa na kuhukumiwa kwa wakristo katika wataifa ya Mashariki ya Kati alisema "leo tuna watu wenye imani thabiti kuliko karne ya kwanza (baada ya kristo)"

Idadi ya wakristo imezidi kupungua nchini Iraqi kutoka idadi ya wakristo milioni 1 na laki 4 mwaka wa 1989 na kwa sasa 400,000 .

Kuanzishwa kwa kikundi cha islamic state kumechangia sana wakristo kukimbia taifa hilo kutokana na vitisho wanavyopata ama gharama wanazotozwa kwa kukataa kusilimu