Mombasa Port operation. Photo/FILE
Maafisa wa polisi wa vikosi vyakupambana na dawa za kulevya wakilinda   Picha na Citizen Digital

Maafisa wa Jeshi la Polisi nchini kenya wanazuilia meli inayoshukiwa kubeba shehena ya dawa za kulevya kwenye badndari ya mombasa.

Kikosi cha maafisa hao, kilijumuisha maafisa kutoka kikosi cha kupambana na dawa za kulevya na maafisa wa uchunguzi wa jinai, kilifika katika bandari hiyo ghafla usiku wa manane(General Service Unit na Recce squad).
Bandari ya Mombasa
Picha ikionesha milango yakuingilia bandarini             Courtesy of BBC-swahili

Maafisa hao waliagiza kila mtu kuondoka na kufunga milango yote ya kuingia na kutoka kwenye bandari hiyo.
Operesheni hiyo iliwashangaza hata wasimamizi wa bandari hiyo walioonekana kutokuwa na habari,watumishi hadi Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya Baandari Kenya Bwana Gichiri Ndua.

Mkuu wa polisi wa Mombasa Francis Wanjohi amethibitisha kwamba wanasaka dawa za kulevya kwenye meli hiyo.