UGANDAN-YOUNG-MAN-WITH-OLD-WIFE PHOTO/SUNDAY VISION
 

Mwanaume mmoja mwenye umri wwa miaka 27 wa asili ya kiganda  Steven Tikubuwana anapanga kufunga ndoa na mpenzi wake mwenye umri wa miaka 70 Bi. Zaituni Nakanda mapema mwaka kesho,kama ilivyoripotiwa na Sunday Vision ya Uganda.

Gazeti hilo limeendelea kufichua kuwa wawili hao wanaishi pamoja katika nyumba ya chumba kimoja inayomilikiwa na Zaituni

Wawili hao walikutana baada ya bwana Tikubuwana kuachishwa kazi yake ya shamba na Zaitun i kumhifadhi kwake.
Tikubuwana anasema "nilipoteza kazi na kwa miezi miwili nilikuwa sina makaazi,ila alinikaribisha nyumbani kwake japo mwanzoni alikuwa na uoga baada akanizoea"

Aliongezea kusema kuwa japo ndugu zake hawajaliafiki swala hilo hatishiki kwa lolote.

Hii itakuwa kuwa ndoa ya pili kwa Tikubuwana baada ya kuachana na mkewe wa kwanza ambae wamejaaliwa watoto wawili mmoja ana miaka nane kwa sasa na mwingine miaka minne,wote ambao wanaishi na wazazi wake katika wilaya ya Kabale.

Kijana huyo ameendelea kueleza kuwa bado hajawataarifu wazazi wwake ila atawapa taarifa kabla ya harusi.

Na kwa upande wa Bi.Zaituni anasema hawajahi kuwa kwenye mahusiano tangu 1993 baada yakumuacha mume wake wa zamani, Zaituni alisema   "Kumpata mume ni muujiza".

Anadai hayamshitui maoni hasi yanayotolewaa kuhusiana na mahusiano yao.

Kwa sasa bi. Zaituni Nakanda anadai kuwa yeye ni mjamzito,jambo lilipingwa na madakatari waliomkagua katika hospitali ya Mulago. Hata na hivyo amekataa kuamini matokeo ya vipimo vya madaktari hao.

Bi.Zaituni ambaye ni mzaliwa wa Wilaya ya Kimulu  hawabahatika kuwa na mtoto maishani mwake,wala kubeba mimba ama kupata hedhi tangu ujana wake.

Ndugu zake hawapo tena hivyo husaidiwa na jamaa zake waliopo Mukono.
Mpenzi wake wa sasa ni kibarua katika Halmashauri ya Mukono, Gazeti hilo limeelezea .

Chanzo:citizen digital