Rais Jakaya Kikwete azindua jengo la PSPF  jijini Dar es salaam
Picha ya PSPF TOWER
Jengo hilo ni kati ya majengo machache marefu barani Afrika na linaongoza Africa Mashariki na kati, kwa urefu wa. Mita 147 lina minara miwili,na ukubwa wa mita za mraba  73,000.
PSPF Tower imegharimu shilingi bilioni 139.20 za Tanzania na ujenzi wake umechukua kipindi cha miaka minne, ndani yake kuna ofisi na nyumba za kuishi 88 pia mgahawa,bwawa la kuogelea,mabenki,sehemu ya kufanyia mazoezi na maegesheo ya magari.