Austria inatarajia kupokea wahamiaji wapatao 10,000 wengi wao wakiwa wakimbizi kutoka nchini Syria watakao ingia nchini Austria  kutokea Hungary.


Usiku wa kuamkia leo wafanyakazi wa Shirika la misaada walipokea watu wengi sana  baada ya  Hungary kutuma mabasi kuwachukua kutoka mpakani. 
Treni maalum zimeandaliwa kuwasafirisha kwenda Vienna.
Serikali ya Budapest imesema hakuna mabasi na treni hii imechangia makundi mengine ya watu waaanze kutembea kwa miguu kutoka mjini kuelekea kwenye mipaka ya Austria.
  
chanzo:BBC-Swahili