Mkuu wa wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo, Ruan Swanepoel
(kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es
Salaam leo asubuhi katika uzinduzi wa kampeni ya ya Chagua Tigo Pesa,
Inalipa. Kulia ni Meneja Bidhaa wa Tigo, William Mpinga.
Meneja Bidhaa wa Tigo, William Mpinga (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo. Kushoto ni Mkuu wa wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo, Ruan Swanepoel.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya simu ya mkononi ya tigo Tanzania imezindua Kampeni
iitwayo"chagua tigo pesa,inalipa"ikiwa na lengo na la kuongeza
upatikanaji wa fedha kwa njia ya simu ya mkononi kwa wateja.
Akizungumza Dar es Salaam jana asubuhi Mkuu wa Kitengo cha Huduma za
Kifedha wa Tigo Ruan Swanepoel alisema huduma hiyo ikiwa na muonekano
mpya na sura kwa wateja wake wanaotumia huduma ya tigo pesa Tanzania
nzima.
Alisema kuwa kwasasa mtandao wa tigo umeenea kwa wingi hapa nchini na
unatumiwa na asilimia 90 ya wananchi wote wanaomiliki simu za mkononi.
Alisema kuwa mtandao wa tigo unakikisha inatoa huduma stahiki kwa wateja
wakena kuhakikisha huduma ya tigo pesa inazidi kuwa na huduma pendwa
kwa sababuinapatikana kirahisi na makini.
Alisema kuwa huduma hii inalipa kwa wateja wake na kukopa fedha hasa kwa wale wenye kipato kidogo na wasio na huduma za kibenki.
Alifafanua kuwa wateja wa tigo pesa watanufaika na kampeni hii kwa
kuypata vifurushi vya bure kila wannunuapo bidhaa na kulipia kwa tigo
pesa kutoka kwa wauzaji waliosajiliwa.
Pia aliongeza na kusema kuwa wateja watapata riba kila baada ya miezi
mitatu kulingana na kiasi cha fedha ya kifurushi ambacho mteja
atamnunulia mtu mwingine kwa tigo pesa.
0 comments