Bmay w
Bondia Mmarekani Floyd Mayweather ametumia pound milioni 3 kununua gari la kipekee duniani. Mpaka sasa magari haya yametengenezwa mawili tu na yeye anamiliki moja.
Floyd aka ‘Money Man’ ameweka picha hii mtandaoni akiwa na gari ya rangi ya silver ya kampuni ya Koenigsegg. Gari hili linaitwa CCXR Trevita.
Picha iliambatana na ujumbe uliosema  ‘My new 4.8 million dollar car, Koenigsegg made only two Trevita’s for the world and this is No.2 of 2.”
Gari hili litakuwa miongoni mwa magari yake ya kifahari yenye thamani ya zaidi ya dola pound milioni 35 ambazo ni sawa na dola za kimarekani milioni 54m. Floyd ana Ferrari 3,  Porsche 1, Lamborghini 1,Bugattis 3 na ndege yenye thamani ya dola milioni $47 inayoitwa Gulfstream V.
may wayher
floyd-mayweather
Chanzo: Mwanaharakati blog