Ukijaribu
kuwahoji wanaume walio wengi endapo wanatamani kuongeza maumbile yao ya
uzazi, kwa maana ya urefu na upana, majibu mengi ni “ndiyo.”
Ni jambo
ambalo limeenea katika jamii nyingi na kuwaathiri wanaume kisaikolojia.
Wengi wanaamini maumbile makubwa ndiyo yanakupa uwezo wa kumfikisha
kileleni mwenza.
Vilevile
huamini kuwa maumbile hayo ndio yanayoleta msisimko kupita kiasi na
kuamini wataonekana rijali na watawavutia wanawake wengi.
Pasipo
kufahamu kuwa msisimko wa kilele cha tendo ni ujuzi wako binafsi,
kutumia akili na kutumia viungo vyako vya mwilini kuweza kuleta
msisimko. Hawajui pia, afadhali kuwa na uume wa wastani kuliko mkubwa
uliopitiliza kwani unaweza kumsababishia maumivu mwenza wake na
asifurahie tendo hilo na anaweza pia kupata hofu kwa ukubwa huo.
Jambo
usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Laiti kama kungekuwa na njia salama
za kunenepesha na kurefusha maumbile katika huduma za afya, gharama za
kuchangia matibabu zingekua maradufu.
Kwa sababu
wanaume wengi wanaodhani wana maumbile madogo ya uume wangemiminika
kwenda kutibiwa tatizo hilo. Wizara ya Aafya na Ustawi wa Jamii na
Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Tanzania (TFDA) na hata zile za nchi
zilizoendelea ikiwamo Uingereza na Marekani na Shirika la Afya Duniani
(WHO), vyuo vikuu vinavyofanya mamia ya utafiti, hakuna mahala
wamepitisha na kupendekeza dawa au kifaa tiba kwa ajili ya kurefusha na
kunenepesha uume kwa watu wazima.
Njia chache
tu ambazo wanakubali kuwa zinaweza kusaidia angalau kidogo kuongeza
lakini isiyozidi nchi moja, njia hizo ni pamoja na kupunguza unene.
Watu wanene
kupitiliza, chini ya kitovu shina la uume humezwa na mafuta na nyama
zingine zilizorundikana na hivyo kupunguza urefu wa uume kutokea katika
shina.
Hivyo
kupunguza unene kwa njia ya vyakula na mazoezi inakubalika. Vilevile kwa
njia za upasuaji ikiwamo wa kupunguza mafuta ya eneo hilo.
Vitu
vinavyojulikana kutumika kiholela kunenepesha na kurefusha uume ni
pamoja na vidonge, sindano, virutubisho, mashine maalumu, upasuaji wa
kupandikiza, vifaa vyakufanyisha mazoezi uume, mafuata, cream za kupaka
uumeni na mitishamba.
Vitu hivi
vinauzwa kisiri katika baadhi ya maduka ya dawa baridi, kwa njia ya
mtandao. Wapo wanaopita mtaani wakizuiza mikononi na wapo wanauza kwa
kujitangaza katika magazeti.
Hata hivyo,
kati hivyo nilivyotaja, hakuna vinavyofanya kazi kwa ufanisi na kukidhi
vigezo vya kitaalamu kupitia vyombo vikubwa vya matibabu na uthibiti wa
magonjwa, likiwamo Shirika la WHO.
Kwa sababu
hakuna tafiti za kisayansi kuthibitisha ubora, ufanisi na usalama wa
vitu hivyo. Ni kweli vingine vinaweza kukusaidia lakini ndio vinakuacha
na madhara makubwa hapo baadaye.
Madhara hayo
ikiwamo kukosa au kupungua nguvu za kiume, kupata michubuko, kuvunjika
misuli ya uume, madhara ya neva na kupata maumivu sugu wakati wa
kujamiiana. Tafiti inaonyesha wanaume wengi wanajikuta wakinasa na
kununua vifaa hivi kirahisi kwa sababu ya kuathirika kwao kisaikolojia,
hujikuta na shauku iliyopitiliza ya kuongeza maumbile. Ukijaribu
kuwadadisi unakuta wengi wao hawajawahi hata kufika huduma za afya
kuomba ushauri wa tatizo hilo. Wengi wanaojihisi wana uume mdogo
hugundulika kuwa hawapo chini ya nchi tatu, baada ya uume kusimama.
Moja ya
tafiti iliwahi kugundua kuwa wanaume wanaotaka upasuaji wa uume ili
kurefushwa, huwa wana tatizo la kiakili lijulikanalo kitaalam penile
dysmorphic disorder.
CHANZO;MWANANCHI
CHANZO;MWANANCHI
0 comments