Korea kaskazini na Kusini zachukua hatua kupunguza wasiwasi kwa wananchi wao kwa kupunguza vikosi vilivyopo mipakani.
Hayo yametukana na mazungumzo yaliyochukua muda mrefu. Nchi zote mbili zilifikia htua yakuthibiti mipaka yao kwa kuweka vikosi baada ya mapigano ya muda mfupi yaliyotokea wiki jana
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa pande zote mbili, Korea kusini imekubali kuacha kueneza  propaganda zinazochochea pande mbili hizo, huku Korea kaskazini ikielezea masikitiko yake juu ya tukio la hivi karibuni la utegaji bomu lililojeruhi wanajeshi wawili wa Korea kusini.
Nchi hizo mbili pia zimekubaliana kufanya tena mazungumzo ya kuimarisha uhusiano wao.
chanzo BBC-swahili