![]() |
Mshukiwa wa Ugaidi Rukia Faraj |
Serikali ya Kenya imetangaza kutoa dau shilingi milioni mbili za kikenya sawasawa na Dola 20,000 kwa yeyote atakayetoa taarifa kuhusiana na mshukiwa wa ugaidi wa kike ajulikanae kama Rukia Faraj.
Mwanamke huyu anasakwa kwa tuhuma zakuwasaka wasichana wadogo kwa kuwapeleka na kuwasajili katika kundi la kigaidi la Alshabaab lilipo Somalia ilikupewa mafunzo yakigaidi.
Mumewe Rukia ajulikanae kwa jina la Ramadhan Kufugwa ambae naye alikimbilia Somalia anasakwa kwa madai yakupanga mashambulizi nchini Kenya
Kundi la Alshabaab limekuwa likiwatumia watu wa kila rika na jinsia mbalimbali ili kutimiza nia yao yakuvuruga amani kwa mataifa ya Somalia,Kenya,Uganda huku hali hiyo ya tahadhari ikitanda hadi mipaka ya Tanzania
Wengine wanaosakwa ni pamoja na Mohammed Kuno anayejulikana kwa jina lingine Gamadere au Dhuliadein ambaye anatuhumiwa kupanga mashambulio ya kigaidi katika chuo kikuu cha Garisa, ambapo zaidi ya watu 148 waliuawa
Chanzo: BBC-Swahili
0 comments