India yaifungulia kesi kampuni ya Nestle ikidai fidia ya $100m kwa uendeshaji mbovu wa biashara,
Madai ni kuwa kampuni Nestle iliwalaghai wateja wake kwa kutumia matangazo yao ya  bidhaa ya Maggi nodddles yaliyowahadaa

Bidhaa hiyo ilikatwaza India na mamlaka ya chakula ya nchi hiyo kutokana na kushindwa kutimiza sheria za usalama wa afya ya binadamu

Nestle imeyakana madai hayo mahakama kuu Mjini Bombay,huku wakisisitiza bidhaa zao ni salama.
Asilimia 80 ya soko la bidhaa ya maggi noodles ipo India ambapo hadi sasa Nestle imeshaenda hasara yakuchoma tani 400 za bidhaa hiyo hadi sasa.

MAGGI NOODLES
Malamiko hayo kwa niaba ya watumiaji wa bidhaa hiyo na raia wa India hayakufikishwa mahakani moja kwa moja ila yalifikishwa kwenye tume ya taifa inayohusika na kushughulikia matatizo ya bidhaa kwa watu wa India 'National Consumer Disputes Redressal Commission (NCDRC)'

Mamlaka ya chakula na ubora ya India .Food Safety and Standards Authority of India (FSSAI) imesema bidhaa hiyo ya Nestle iligundulika kuwa ni hatari kwa afya ya binadamu kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha aina ya madini ya Lead.

Nestle imeendelea kujitetea kuwa bidhaa zao ni salama kama utafiti unavyoonesha nchi zingine kama Uingereza na Singapore
Maabara mbili nchini India Jimbo la Magharibi la Goa,na Mji wa kusini Mysore imeidhinisha bidhaa hiyo lakini bado mamlaka ya chakula inamashaka na vipimo hivyo

Uamuzi wa mahakama kuu ya Bombay unatarajiwa kutolewa hivi karibu.Mahakama hiyo imependekeza bidhaa hiyo kupimwa tena kabla ya hukumu.