http://i2.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2015/08/UKAWA-II.jpg
Picha: Waziri mkuu mstaafu Mh. Sumaye akihutubia waandishia wa habari wakati akitangaza kuhamia Chadema

Waziri mkuu mstaafu wa awamu ya tatu Frederick Tluway Sumaye ametangaza rasmi kujiunga na umoja wa vyama vya UKAWA leo jijini Dar es salaam.

Frederick Tluway Sumaye alitumikia miaka kumi kwenye nafasi ya Uwaziri Mkuu wakati Mzee Benjamin William Mkapa akiwa Rais wa Tanzania kuanzia mwaka 1995 hadi 20005 alipopisha uongozi wa awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Edward Ngoyai Lowassa akiteuliwa kuwa waziri mkuu na kisha kujiuzulu baada ya muda mchache kutokana na kashfa ya Richmond.

Mzee Sumaye alisema kuwa yeye ni mmoja wa Makada wa CCM waliochukua Fomu kuwania kupitishwa kwenye nafasi ya Urais CCM lakini hakufanikiwa kupita kwenye nafasi hiyo akiwa na lengo la kurekebisha Utawala na kujenga Chama mbadala wa CCM jambo liloshindikana kutokana na kushindwa kupitishwa kwa nafasi hio.

"Natoka CCM ili kuimarisha Upinzani na wala sijiungi na UKAWA kwa maslahi binafsi na sijadai fedha wala cheo.Natangaza rasmi kuhamia UKAWA, kuhusu Chama gani nitawaambia baadaye. Asanteni sana."


Na Raphael Ebacha