Katibu Mkuu wa Chadema,Dk.Wilbroad Slaa


Wakati vyama vya upinzani vikijiandaa kuzindua kampeni zake katika uwanja wa Jangwani hapo kesho ili kumnadi mgombea wake wa urais, Mh. Edward Lowassa, duru zinaeleza kuwa huenda Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa akahudhuria uzinduzi huo.

Mmoja kati ya viongozi wa Chadema ambaye alinukuliwa na gazeti moja kubwa nchini huku akitaka jina lake lifichwe, alinukuliwa akisema “Zipo taarifa za chinichini kuwa Dk. Slaa atahudhuria uzinduzi, hatujui zina ukweli kiasi gani na atashiriki kama Katibu Mkuu au mgeni mwalikwa, kama atahudhuria, atatusaidia sana na asipokuja suala lake litaendlea kuwachanganya wafuasi wa Chadema,” alinukuliwa kiongozi huyo wa Chadema.

Haijafahamika kama taarifa hizo ni za kweli au uzushi ila kwa kuwa hata uamuzi wa kumkaribisha Edward Lowassa kujiunga na Chadema ulifanywa kuwa siri kubwa kwa viongozi wachache sana takribani miezi mitatu kabla. 

Dk. Slaa alijiweka kando na harakati za kampeni za Chadema na Ukawa kwa ujumla baada ya kutoridhia uamuzi wa chama chake kumkaribishaLowassa ambaye awali walikuwa wakimtuhumu kuwa katika orodha ya mafisadi nchini.

Ukawa wanatarajia kufanya uzinduzi wao kesho (Agosti 29) katika viwanja vya Jangwani ikiwa ni wiki moja baada ya CCM kuutumia uwanja huo kwa shughuli hiyohiyo.

chanzo:PressTz