Msanii wa Hiphop kutoka nchini Kenyan almaarufu kama Octopizzo amegeuka kuwa mada katika mitandao mbalimbali yakijamii

hii imetokana na msanii wa miondoko ya RnB kutoka marekani August Alsina kupitia usimamizi wake kuandika katika account yake ya mtandao wa Tweeter kutoshirikishwa kwenye wimbo mpya wa Octopizzo ujulikanao kama THIS COULD BE US

Maneno kutoka mtandao wa Tweeter ya msanii huyo yalikuwa kama ifuatavyo "FROM MANAGEMENT: "The song 'Could Be Us' by Octopizzo does not feature  August Alsina"-Mgmt"

Octo ambae kwa muda amekuwa na bifu na msanii mwenzake Kaligraph kwa muda sasa alionekana kutulia kwa muda huku Kaligraph akizidi panda ngazi na umaarufu wake kuongezeka

Wadau wa muziki wamesema inawezekana ikawa mojawapo ya njia zitakazomrudisha msanii huyu ambae kwa muda sasa amekuwa kimya katika kutawala Chati ya muziki wa Hiphop Kenya na Afrika Mashariki.
Kipindi hiki cha uzinduzi wa albamu yake mpya

Kwa njia hii Octopizzo amepata nafasi kusikilizwa kimataifa na wadau mbalimbali wasiomfahamu kutaka kuijua nyimbo yenyewe na msanii husika na kuongeza mauzo ya albamu yake mpya LDPC (Long Distance Paper Chasers ) ambayo amekuwa mtu wa tatu toka Afrika Mashariki kuipost kwa mtandao wa muzikiwa Jay-z wa TIDAL wengine wakiwa ni Erica na Wakazi
tidal-share.e86656fe