Katibu mkuu wa chama cha ACT Zitto Kabwe amese kuwa watazindua kampeni zao Jumapili hii katika ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es salaam.

Kiongozi wa Chama cha ACT-Tanzania, Zitto Kabwe
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Zitto amesema kuwa chama hicho ndicho chama cha pekee chenye sera nchini na vipaumbele vya chama hicho kwa mwaka huu ni vinne tu navyo ni; haki ya Watanzania kwenye hifadhi ya jamii, kila Mtanzania kuwa na bima ya afya, uchumi unaozalisha ajira na afya pamoja na elimu kwa ajili ya nchi yetu.
  
"Tunapenda kuwaambia kuwa katika majimbo 265 ya Tanzania, ACT imesimamisha wagombea 219 wa Ubunge, hii inafanya chama chetu kuwa cha pili kwa idadi kubwa ya wagombea Ubunge nchini baada ya CCM ambayo imesimamisha wagombea 265 nchi nzima, CHADEMA wagombea 138, ikifuatiwa na CUF na vyama vingine," Alisema Zitto.

 "Chama chetu ndio kinachoongoza kwa idadi ya wagombea Ubunge wanawake ambapo 25% ya wagombea ni wanawake pia chama chetu ndio chama cha kwanza kusimamisha vijana wawili wenye umri chini ya miaka 25 nchini na tumeenguliwa jimbo la K'ndoni bila sababu za msingi eti kisa mgombea wetu hajadhaminiwa, tumekataa rufaa NEC na pia mgombea wetu jimbo la Singida Mashariki kakatiwa rufaa na Tundu LISSU kwa sababu zisizoeleweka," Aliongeza Zitto